Sunday, February 17, 2013


KUKOSA HAMU YA KULA KWA WATOTO!

kukosa hamu ya kula huwatokea watoto wengi hasa wale wenye umri kati ya miaka 2-6. Wazazi huwa na wasiwasi sana mtoto wao asipokula vizuri,lakini tatizo hili husababishwa na nini? kama mtoto hana ugonjwa wowote basi sababu huwa hii
  • kwa kawaida mtoto anapofikisha umri huo huwa ukuaji wake (rate of growth) hupungua na mahitaji ya virutubisho vya mwili (nutrition requirements) pia hupungua.Wakati huu watoto huwa wanaanza kujifunza kujitegemea kwa kuanza kuchagua vile wanavyovipenda na vile wasivyovipenda.ni vizuri kutambua hii ni kawaida kwa watoto katika umri huu!

Wednesday, February 13, 2013

Tuesday, February 5, 2013

BREASTFEEDING POSITION,THE RIGHT AND THE WRONG


UMUHIMU WA MAZIWA YA MAMA! UNASEMAJE

  • Watoto wanaonyonya maziwa ya mama hupata kinga nzuri dhidi ya magonjwa mengi kama kisukari,kansa na magonjwa ya moyo.
  • Maziwa ya mama humsaidia mtoto asipatwe na magonjwa ya kuhara.
  • Humsaidia mtoto asipatwe na magonjwa ya meno kama kuoza. 

Saturday, February 2, 2013

MYSELFAND I


DAWA BARIDI NA MAFUA! WATOTO JE!

Wataalamu wanashauri kutotumia dawa baridi (over the counter) kutibu magonjwa ya kikohozi na mafua kwa watoto wadogo. Tafiti zinaonesha kwamba hazisaidii kupunguza dalili za ugonjwa kwa watoto wenye umri mdogo. Na huweza kuwa  sumu, hasa pale ambapo hutumika zaidi ya dose iliyowekwa(over dose) .

MAFUA NA KIKOHOZI KWA WATOTO! WHAT DO U THINK!


MAFUA NA WATOTO! UFANYE NINI UKIWA NYUMBANI?

Mafua kwa watoto limekuwa tatizo linalowasumbua wakina mama wengi! unaweza kuanza kufanya yafuatayo ili kumsaidia mtoto!
  • muweke mtoto apumzike sehemu yenye hewa ya kutosha na salama kama kitandani
  • mpe fluids(maji,au juice ya matunda) kwa wingi hasa yenye Vitamin C
  • anapokuwa na joto mpatie paracetamol (panadol) badala ya aspirin
  • atahitaji uangalizi wa karibu au mpeleke kwa daktari kama kuna yafuatayo            
                                 -  mtoto wako ni mdogo chini ya mwezi mmoja
                                 - ana mafua mazito ambayo yanamkosesha kupumua vizuri
                                 - mafua yanatoka mfululizo kama maji